KITIVO CHA SANAA NA SAYANSI YA JAMII
IDARA YA LUGHA NA ISIMU
TLK
521: SINTAKSIA YA KISWAHILI
Kazi
ya Pili
Maelekezo
- kazi ifanywe na kundi la wanafunzi kumi na tano, na kila mwanafunzi ashiriki kikamilifu.
- kazi hii inauzito wa alama 10
- kazi ichapwe kwa mwandiko wa Times New Roman, nafasi iwe 1.5
- kazi itakusanywa siku ya Ijumaa tarehe 17/01/2014 saa 11:00 – 8:00 mchana.
Swali
MWALIMU ANATUTAKA TUFAFANUE TENA KWA KINA DHANA HIZI NA SI TUELEZE
ReplyDelete1.Viambajengo ni vijenzi katika sentensi ambavyo hushirikiana na vingine ili kujenga vipashio vikubwa zaidi.
2.Utawala wa kiuambajengo ni hali ya kifundo cha kijenzi kimoja kukimiliki kifundo kingine.
3.Kutawala kwa karibu ni hali ya kifundo kikubwa kukimiliki vifundo vingine pasi ukingo kati yake.
4Mahusiano ya kutangulia ni hali ya neno au kifundo kimoja kujitokeza kabla ya kingine katika ulalo. Yaani kinachokuwa kushoto kinakitangulia kilicho kulia.
5.Kifundo mama ni kifundo ambacho kinamiliki vifundo vingine. Mfano S ni kifundo mama cha KN na KT.
6.Kifundo binti ni kile ambacho kinamilikiwa kwa karibu na kifundo mama. Kwa mfano KN na KT ni vifundo binti vya S.
7Kifundo dada ni kile ambacho kinahusiana na kingine kwa sababu ya kuzaliwa au kumilikiwa na kifundo sawa. Kwa mfano kifundo KN ni dada kwa KT.